VIWAWA 107 TOKA PAROKIA YA K/NDEGE WATEMBELEA JIMBO LA MOROGORO.

Viwawa kutoka Parokia ya Mwenyeheri Beatha Maria Theresa Ledochoska, Jumapili ya tarehe 31/01/2016 walitembelea Jimbo la Morogoro, Parokia ya Petro na Paulo, GAIRO. Walikuwa viwawa 107 ambapo safari yao ilianza saa 12:40 Asubuhi kutokea Parokiani K/ndege na waliwasili Parokiani Gairo saa 3:04 Asubuhi, walianza kwa maadhimisho ya Ibada Takatifu iliyoongozwa na Baba Paroko wa Parokia ya Petro na Paulo. Alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha vijana juu ya kujitoa kikamilifu katika utume pia alikumbusha kwamba siku hiyo ni kumbukumbu ya Mt. Don Bosco na kusema kuwa alipenda sana vijana siku za uhai wake na mpaka leo hii bado ni mwombezi wa vijana, wamemuenzi Mt. Don Bosco kwa kujenga vituo mbalimbali na mashule kwa ajili ya kuelimisha vijana kwa nchi tofauti tofauti duniani ikiwemo na Tanzania kwa mkoa wa
Dodoma kuna chuo cha ufundi na shule ya seminary.
Mada mbalimbali walizoshirikishana vijana.
- Namna ambavyo kijana anaweza kutengeneza wazo la biashara itakayokuwa na faida kwake.
- Maadili ya vijana kutoridhisha ndani ya kanisa na jamii kwa ujumla.
Pia baada ya ratiba za Mada tulizoshirikishana kilichofuata ni vijana walielekea uwanjani na kushirikishana kwa njia ya Michezo ya Football na Netball.
0 comments:
Post a Comment