Saturday, February 6, 2016

VIWAWA 107 TOKA PAROKIA YA  K/NDEGE WATEMBELEA JIMBO LA MOROGORO.


Viwawa kutoka Parokia ya Mwenyeheri Beatha Maria Theresa Ledochoska, Jumapili ya tarehe 31/01/2016 walitembelea Jimbo la Morogoro, Parokia ya Petro na Paulo, GAIRO. Walikuwa viwawa 107 ambapo safari yao ilianza saa 12:40 Asubuhi kutokea Parokiani K/ndege na waliwasili Parokiani Gairo saa 3:04 Asubuhi, walianza kwa maadhimisho ya Ibada Takatifu iliyoongozwa na Baba Paroko wa Parokia ya Petro na Paulo. Alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha vijana juu ya kujitoa kikamilifu katika utume pia alikumbusha kwamba siku hiyo ni kumbukumbu ya Mt. Don Bosco na kusema kuwa alipenda sana vijana siku za uhai wake na mpaka leo hii bado ni mwombezi wa vijana, wamemuenzi Mt. Don Bosco kwa kujenga vituo mbalimbali na mashule kwa ajili ya kuelimisha vijana kwa nchi tofauti tofauti duniani ikiwemo na Tanzania kwa mkoa wa Dodoma kuna chuo cha ufundi na shule ya seminary.  

Mada mbalimbali walizoshirikishana vijana.


  1. Namna ambavyo kijana anaweza kutengeneza wazo la biashara itakayokuwa na faida kwake.
  2. Maadili ya vijana kutoridhisha ndani ya kanisa na jamii kwa ujumla.


Pia baada ya ratiba za Mada tulizoshirikishana kilichofuata ni vijana walielekea uwanjani na kushirikishana kwa njia ya Michezo ya Football na Netball.


K/NDEGE WAPOKEA UGENI MZITO WA VIJANA TOKA JIMBO LA NAIROBI, KANGEMI, KENYA.








Vijana 15 kutokaJimbo Kuu Katoliki la Nairobi, Parokia ya Yoseph Mfanyakazi iliyoko Kangemi, Nairobi KENYA. Walitembelea viwawa wa Parokia ya K/ndege ili kushiriki nao sikukuu ya christmass ya vijana, waliwasili Jumatano tarehe 23/12/2015 na kushirikishana mambo mbalimbali hasa yanayohusu utume wa vijana na walikaa pamoja mpaka tarehe 28/12/2015. Mada mbalimbali ziliendeshwa na  Michezo ya pamoja, ilikuwa ni furaha kwa kukutanisha vijana toka mataifa mawili tofauti kwao ilikuwa ni furaha tosha kwa kuwa pamoja na walidumisha Mapendo Daima kama vijana wakatoliki.

















Thursday, February 4, 2016

KONGAMANO LA VIWAWA JIMBO KUU KATOLIKI LA DODOMA


Katika kuhakikisha kunakuwepo na umoja imara wa viwawa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Utume wa viwawa Jimbo kwa kushirikiana na walezi wake waliandaa Kongamano la viwawa Jimbo lilofanyika Parokiani Veyula kuanzia tarehe 02-07/12/2015, lililoshirikisha vijana 200 toka katika kona ya Dekania zinazounda Jimbo kuu Katoliki la Dodoma, ambako kwa Parokia ya K/ndege ilitoa uwakilishi wa vijana 20.

Mada mbalimbali zilizofundishwa.
  1. Urafiki na Uchumba
  2. Ndoa
  3. Kijana na Maisha ya familia
  4. Miito
  5. Ujasiliamari
  6. Uhai (Pro life)
Pia kulikuwako na fursa mbalimbali za kushirikishana vijana kwa njia ya michezo ikiwemo, Mpira wa Miguu, Mpira wa pete ( Netball), Kucheza miziki mbalimbali na Mashindano ya kusoma Biblia.

  Hao ni baadhi ya vijana wakiwa sambamba kabisa kwa utulivu wakipata semina zinazoendelea.






Wakati sista alipokuwa akiendesha Mada ya Uhai (Pro life), akizungumzia masuala ya vizibiti mimba kwa vijana wa kike.  


Wito kwa vijana (viwawa) wote kushiriki shughuli zote hasa makongamano ili kupata Semina na kujifunza zaidi juu ya Imani yetu katoliki.

Friday, September 11, 2015

KILELE CHA MAADHIMISHO YA KONGAMANO LA VIJANA WAKATOLIKI


ASKOFU wa Jimbo la Kuu la Songea mkoani Ruvuma, Damian Dallu akizungumza wakati wa misa maalum ya maadhimisho ya kilele cha kongamano la vijana wakatoliki kitaifa mjini Njombe 




Vijana wakatoliki kutoka mkoani Iringa wakiwa katika maandamano
Na Mwandishi Wetu 
ASKOFU wa Jimbo la Kuu la Songea mkoani Ruvuma, Damian Dallu amesema vijana wengi wamekuwa wakikosa ajira na kubaki wakilalamika kutokana na wazee wengi kuendelea kung’ang’ania madaraka na kugoma kustaafu jambo ambalo linaendelea kusababisha chuki miongoni mwa vijana hao.
Akizungumza jana katika misa maalum ya kufunga kongamano la Vijana wakatoliki Tanzania (VIWAMA) lililofanyika mkoani hapa na kuwakutanisha vijana mbalimbali kutoka majimbo 32 kati ya 34 nchini askofu Dallu alisema wazee ndio wanatakiwa kutumia busara kwa kuanza kustaafu kwa hiari badala ya kusubiri kuondolewa kwa nguvu.

“ukitaka kufanya kazi fanya, usingojee kuheshimika leo, utaheshimika baadaye ukitoka, na hili nalisema kwa wale wanaopenda madaraka hawataki kutoka, inaumiza kabisa, ukichukua wengine pale watahama hawatakuwa na wewe uliyepita zamani, watakuona ni mwema,” alisema Dallu.
“…ukiwa paroko au padre unafanya kazi pale mahari usingoje pale wakuambie baba umefaulu sana, nakuambia ni kazi bure, acha waseme baadaye wakati haupo, na watakuwa wanalinganisha na aliyepo,” alisema.
Askofu Dulla alitumia muda huo kumzungumzia Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kusema alielewa baada ya kufariki dunia kuwa yeye ni nani katika safari yake ya kuwa kiongozi nchini.
“MWalimu Nyerere ameeleweka alichofanya baada ya kufa kwa hiyo ndugu zangu msiogope kuondoka madarakani, mfurahi yale yote mishale inapowaingia mkitoka itatoka, yatabaki makovu,” alisema.